Showing posts with label Love General. Show all posts
Showing posts with label Love General. Show all posts

Tuesday, 13 September 2016

Alama 7 kwamba mumeo anafurahia ndoa yenu


Je, unataka kujua kama mumeo anaifurahia ndoa yenu? Famasia ya Ndoa Maridhawa imekuandalia orodha hii ili uangalie namna unavyoweza kuamiliana vizuri na mumeo. Kisha usiache kuwa mwenye kushukuru kwa kila jema analolifanya.

Kila mke anataka mumewe afurahie ndoa yao. Zifuatazo ni ishara na alama 7 zinazoonesha kuwa mumeo anafurahia kuwa mwanandoa:

1. BUSU
Anakupokea kwa busu anapoingia nyumbani kutoka kazini. Sio busu na haraka haraka kama mtu anayekimbizwa. Ni busu maridhawa, anakukumbatia, anakubusu kwenye kinywa chako au nyama kwa nyama. Hilo linaonesha kuwa anafurahia tena kuwa pamoja na wewe nyumbani. Hakika hiyo ni ishara ya kwamba anafurahia ndoa yenu. 

2. MAWASILIANO
Mume anapotoka nyumbani kwa ajili ya shughuli zake, anawasiliana nawe kila mara na kukujulisha namna alivyo na shauku nawe. Kwa kawaida mume mwenye furaha kwenye ndoa huwa na shauku na mkewe kila anapokuwa safarini au nje ya nyumbani. Huwa na shauku mno ya kuwa pamoja nawe. Mambo atakayokwambia kwenye simu yataonesha jinsi alivyokukumbuka. Hufanya hivyo kwa dhati ya moyo wake. Daima huwa mwaminifu kwako kwa asilimia zote. Hata wewe unalijua hilo.

3. "NINAKUPENDA"
Hukwambia anakupenda. Hulisema neno hilo kila siku, na wewe humjibu. Neno hilo halichuji midomoni mwenu. Sio kama wanaume ambao wake zao hulalamika baada ya miaka mingi ya ndoa, “Huniambii kama wanipenda”, nao wakajibu, “Nilikwambia tulipooana, na kama mambo yakibadilika nitakwambia.” Hivyo sivyo mume mwenye kufurahia ndoa yake anavyofanya. Atakwambia anakupenda kwa sababu anataka ulijue hilo kila siku. Anapenda kusema hivyo kutoka moyoni mwake. Na anajua kwamba unafurahia na ni muhimu kwako kulisikia neno hilo.

4. ANAKUSAIDIA
Miongoni mwa alama za kuwa anaifurahia ndoa yenu ni kukusaidia mambo ya nyumbani. Anataka kukuangazia njia yako na kushirikiana nawe, kiasi kwamba anaweza kufanya zaidi unapokuwa hujisikii vizuri. Ni mwenza mwenye utashi katika shughuli za kuifanya nyumba yako kuwa sehemu maridhawa. Anatambua kuwa kulea watoto sio kazi yako peke yako, bali ni yake pia; yuko tayari kushirikiana nawe kwa sababu anakupenda na anawapenda pia. Kwa maneno mengine, ni mshiriki hai katika kuyafanya maisha ya nyumbani kuwa yenye furaha kwa familia yake.

5. HUKUSTAAJABIA
Mume mwenye furaha na ndoa yake hukusifu. Hukutazama na kuangalia unachofanya. Huwa makini, na utamuona mara kwa mara akikutazama na kufurahia unachokifanya. Anavutiwa na wewe, na hachoki kukutazama. Huendelea kukuona kuwa u mrembo hata kama mwili wako utabadilika kiasi gani. Haoni kasoro unazoziona. Amekuwa kipofu wa upendo na mahabba.

6. HUKUFARIJI
Hukukumbatia unapolia. Huzuni na mfadhaiko vinapokusibu na kukufanya ulie, hukufariji. Hufanya juhudi kujua tatizo linalokusibu. Daima hukupa faraja katika nyakati ngumu. Kama una busara, utaikaribisha faraja yake na kuipokea. 

7. HUUFUNGUA MOYO WAKE
Hukushirikisha ndoto zake na changamoto zake. Sio rahisi kwake kufanya hivyo kama sio kwa ajili yako. Anahitaji kujua kwamba anaweza kukwambia mambo hayo bila kukusumbua, na kwamba utamuunga mkono na kumfanya ajiamini. Anapokuwa tayari kuunfungua moyo wake na kukwambia mipango na matarajio yake kuhusu shughulizake, anatambua kuwa utasikiliza na kujali. Anatambua kuwa wewe ni shabiki wake namba moja. Anajua pia kwamba upendo wake kwako ni wa dhati na utakufanya uelewe na kutaka kujua kuhusu wasiwasi wake. Mume mwenye furaha katika ndoa yake anaweza kufanya hivyo kwa kujiamini kabisa.

WITO
Wito wangu kwa wanaume wanaosoma somo hili tamu: Iwapo hamfanyi haya, sasa ni wakati wa kuanza kuwafanya wake zenu kuwa vipaumbele vyenu. Hamjachelewa kutengeneza furaha katika ndoa zenu. 

Wito wangu kwa wanawake wanaosoma somo hili, furahieni mazuri yote yanayofanywa na waume zenu. Pia wafanyeni kuwa vipaumbele vyenu, mtakuwa miongoni mwa wanandoa wenye furaha watakaoithibitishia dunia kwamba ndoa na furaha ni mapacha wasiotenganishwa, hata katika nyakati ngumu.

Monday, 12 September 2016

Wanandoa kutumia tendo la ndoa kama silaha ni ujinga.


Kuna wanandoa wanaishi maisha ya ajabu sana mathalani unaweza ukamkuta Mwanamke anatumia tendo la ndoa kama sehemu ya kujihami na kufikishia hisia zake kwa mumewe Mara kwa Mara na kuna wakati anaamua hata kumnyima mwenzi wake anapohitaji ili mradi tu aweze kufikisha hoja take mezani.

Hii ni kwa pande zote lakini upande wa Dada zetu ukifuatilia utagundua kuna tofauti.

Kufanya hivyo ni utoto wa tafakuri na kujiharibia taratibu,ni kama kujilipua mwenyewe.

Unamkuta MTU hakuambii chochote ila mkiwa kwenye burudani anakuibulia hoja ya ajabu inayofikia hatua ya kuharibu kabisa mkururo wa hisia za raha Kiswahili cha mitaani wanasema "anakukata stimu"huu ni ujinga mkubwa sana kama ukiendelezwa ni rahisi sana wanandoa kuchokana na kutofurahia tendon la ndoa ambalo ni zawadi yao wote.

Tubadilike zama zimebadilika sana.

What is Love?



1. A strong feeling of affection.
"babies fill parents with intense feelings of love"
synonyms: deep affection, fondness, tenderness, warmth, intimacy, attachment, endearment; devotion, adoration, doting, idolization, worship; passion, ardour, desire, lust, yearning, infatuation, adulation, besottedness

"his friendship with Helen grew into love"
compassion, care, caring, regard, solicitude, concern, warmth, friendliness, friendship, kindness, charity, goodwill, sympathy, kindliness, altruism, philanthropy, unselfishness, benevolence, brotherliness, sisterliness, fellow feeling, humanity

"their love for their fellow human beings" 
relationship, love affair, affair, romance, liaison, affair of the heart, intrigue, amour
"he is confident that their love can survive"

2. A  great interest and pleasure in something.
"his love for football"
synonyms: liking, weakness, partiality, bent, leaning, proclivity, inclination, disposition; enjoyment, appreciation, soft spot, taste, delight, relish, passion, zeal, appetite, zest, enthusiasm, keenness, predilection, penchant, fondness
"her love of fashion"
verb

3. Feel deep affection or sexual love for (someone).
"do you love me?"
synonyms: be in love with, be infatuated with, be smitten with, be besotted with, be passionate about; care very much for, feel deep affection for, hold very dear, adore, think the world of, be devoted to, dote on, cherish, worship, idolize, treasure, prize; informalbe mad/crazy/nuts/wild/potty about, have a pash on, carry a torch for..... "I love you, Rory"